Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Wednesday, April 3, 2013

Sababu Kuu tatu kwanini Wanaume wanataka kuchiti!

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/03/black-man-cheating.jpg
Jamaa anakula chabo…..
Mtaalam wa masuala ya mapenzi, Keith Brown, anasema wanaume, ambao wapo kwenye mahusiano thabiti wanataka kuchiti (kufanya ngono nje ya wapenzi wao) kutoakana na sababu kuu tatu zifuatazo:
# 1 Hakuna furaha ya kutosha maishani mwao. Mwanaume anayetaka kuchiti, huwa anafikiri kwamba yeye ni bora zaidi ya mwanamke aliyenae. Hufikiri kwamba anaweza akapata mwanamke bomba zaidi ya aliyenae. Hivyo basi, siku zote anakuwa na tama za kutafuta mwanamke huyo.
#2 Anakuwa na fikra za kuchiti wakati ushababi wake umejeruhiwa. Wanaume wengi wana amua kuchiti kutokana na hisia kwamba wanawake zao hawawaheshimu, hawawapi umuhimu mkubwa, hawawahitaji kimoyo au kimapenzi, au heshma ya mwanaume imejeruhiwa kutokana na tabia za mwanamke wake.
#3 Sababu ya tatu na ya mwisho kwanini wanaume wanataka kuchiti inafunga ukurasa wa sababu zote zilizotangulia. Ni kwamba, wanaume wanaotaka kuchiti huwa wanafikiri hawatoweza kukamatwa! Hivyo basi wanafikria na hatimaye wanatenda, lakini siku ya siku yana wakuta yaliyo mkuta Tiger Woods, Eliot Spitzer, na wengineo wengi tu…………….

No comments: