Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Comedy

Vichekesho vya mke na mume kanisani
Vichekesho vya mke na mume kanisaniKulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu pale Dar. walikuwa wakisali kanisa moja la kipentekoste.  Mwanaume alikuwa na tabia ya kulala usingizi kila akiingia ibadani. Siku moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani. Unajua ni dawa gani hiyo?
Mke alimminya kwa haraka akamwambia,
“Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa maombi”
Mume akasimama haraka na kuanza kushusha maombi makali ya kufunga ibada
“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa ibada nzuri, na ya miujiza. Tunaomba ututangulie tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika, Amen”
Baada ya kumaliza ibada, alijikuta kanisa nzima likimkodolea macho huku wengine wakicheka sana, na wengine wakiwa midomo wazi na wengine wakiinama kwa aibu.
Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake yaliendelea kuwa mazuri au la...

Hivi yesu atarudi kweli?

Siku moja mlevi mmoja alikaa na kuskuti mara akapata swali la kumuuliza mlevi mwenzie. Na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mlevi 1: Hivi kweli yesu atarudi?mbona cku zinaenda tu?
Mlevi 2: Kwa kipigo alichokipata, hata kama ungekuwa wewe ungekubali kurudi?

Duh! wewe kweli mzigo!     

Mwalimu alikua darasani akamuuliza mzigo swali mazungumzo yalikuwa hivi
Mwalimu: mzigo nikikupa sungura wawili halafu nikakuongezea tena wawili na nikakuongezea tena wawili utakuwa na sungura wangapi?
Mzigo: saba
Mwalimu: sikiliza tena mzigo usiwe na haraka… (Mwalimu akarudia tena vile vile)
Mzigo: saba
Mwalimu: na je nikikupa machungwa mawil nikakupa tena mawil na nikakupa tena mawil utakuwa na machungwa mangapi?
Mzigo: sita
Mwalimu: sasa na je nikikupa sungura wawil halafu wawil tena na wawili tena utakuwa nao wangapi?
Mzigo: saba
Mwalimu: mmh kwa nini?
Mzigo: kwa sababu nyumbani nina sungura mwingine mmoja
Mwalimu: daah wewe kwel mzigo


 

No comments: