Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Wednesday, September 5, 2012

TANZANIA YAENDA WAPI SASA?

WANANCHI WATALIA MPAKA LINI,KWANINI TUNAUANA WENYEWE KWA WENYEWE? 
Tanzania kila siku tunaambiwa na kusifiwa kuwa ndio kisiwa cha Amani lakini imekua ni kinyume. Tanzania imekua sio nchi ya amani tena na haki imepotea kutokana na vitendo vinavyoendelea kufanywa na vyombo vya dola ambavyo vilitakiwa kutetea haki na maslai ya wananchi. Tumeambiwa Jeshi la Polisi ndio mikono salama kwa wananchi wa kawaida linapotokea jambo lolote lenye utata lakini ni kinyume na matarajio ya wengi kwani sasa Polisi ndio wamechukua jukumu la kutuangamiza kutokana na nafasi zao. Kulikua na sababu gani kumuua mwandishi wa habari aliyekua anakiwakilisha kituo cha Channel Ten mkoani Iringa Marehemu Daudi Mwangosi ambaye alikimbilia mikononi mwa Polisi akiamini ndio sehemu salama kwake lakini Polisi wakampiga na mwisho wa siku wakamuua kwa kumpiga bomu. Je,haya mabomu wamepewa ili watulize ghasia au kulipulia wananchi?..
Nadhani kwa hili mmetukosea sana wananchi na hatuna budi kuwaambia  Jeshi la Polisi kuwa hatuna IMANI na nyie tena kwani mnatuua baada ya kutulinda na kwa maana hiyo mnaashiria wananchi wachukue sheria mikononi kwani imani imepotea kwenu.
Kwenye picha ya tukio kama hili kweli inahitajika Tume?
 
Jamani serikali msifikiri bado watanzania wa sasa ni kama wale wa zamani, kama mnavyoelimisha jamii kuwa ibadilike basi na nyie mbadilike kwanza. Tume ya nini katika picha kama hii, ni askari Polisi ambao wanafahamika na wanaonekana kabisa wakifanya kitendo hiko cha kinyama ambacho si kizuri katika Taifa letu ambalo kila siku tunaimbwa kuwa ni kisiwa cha amani. Serikali sio kila jambo muunde tume kwani mambo mengine yanajionesha wazi tu mfano wa hili lililotokea Iringa la mauaji ya mwandishi. Ili turudishe imani kwenu serikali basi hamna budi kuchukua hatua za haraka na waliofanya kitendo hiki cha kinyama wachukuliwe hatua kali ili iwe funzo kwa wengine
Watanzania washaanza kuchoka na serikali isisubiri watanzania wasimame na kusema tumechoka bali wajirekebishe kwanza wenyewe.
Kwa hili nadhani mtatuelewa na serikali ifanye wananchi wanachotaka kwani wapo aple kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
                   Asanteni na Mungu awatie nguvu wafiwa wote na wananchi wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.. Ameen.

No comments: